Nimeamua kuandika blog entry hii kwenye Kiswahili badala ya
Kiingereza kwa hiyo….itakuwa entry fupi!
Nimefika salama Tanzania baada ya kukwama Amsterdam kwa
masaa 24. Kulikuwa na shida na
ndege na kulikuwa hakuna ndege nyingine kwa hiyo lazima tubaki Amsterdam siku
moja. Nikakaa usiku hotelini
nikarudi kituo cha ndege asubuhi.
Mara hii kila kitu kulikuwa poa na tulikuwa njiani Kilimanjaro. Nikaangalia filamu tatu na episode chache
za tv shows alafu tukafika KIA saa 5:35 usiku.
Baba Ngowi na mtoto wake Ema wakanipeleka nyumbani Maji ya
Chai si mbali kutoka KIA. Lakini
niliogopa kusafiri na gari imechelewa sana na hakuna taa barabarani na siku
hizi nadhani Tanzania imekuwa hatari kuliko zamani. Nimesikia habari za watu walioibiwa vibaya au hata
walioua. Baba akaniambia hakuna
shida kwa sababu akaleta bunduki yake ijapo akakaribisha hatari wakati
akasimama gari kuchimba dawa!
Nikamwomba kusubiri tufike nyumbani kwangu lakini nadhani hakuweza kungoja…. Ningalisemaje? Mara nyingi nimesikia hivyo….!
Siku iliyofuata nikateseka sana ya uchovu sikuweza kwenda
Moshi kwa New Year’s kama nimechopanga.
Ilikuwa haiwezekani kabisa.
Afadhali nikabaki nyumbani kuangalia “Real Housewives of Beverly Hills”
kwenye laptop na kula cheese na kunywa mvinyo nimezonunua Schiphol Airport
Amsterdam. Ilikuwa uamuzi safi
kabisa na nikasherekea mwaka mpya na starehe.
Tangu siku ile majukumu yamekuwa mengi na nimekuwa busy sana
na kuweka mambo safi nyumbani na kujizoea tena Tanzania bado natamani kwenda
Moshi wikiendi. Nitakutana na Baba
alafu labda kupita Glacier kwa bia moja (au mbili….) Nitarudi Maji ya Chai Jumapili na kukaa wiki ijayo
Arusha. Blog entry itayofuata
itakuwa kwenye Kiingereza kama kawaida.
Hii hapa ni jaribio tu ili nione kama bado naweza kutunga sentensi ya
Kiswahili.
Sasa, nihukumiwe.
Naomba kwamba Waswahili wanaosoma hii post, tafadhali nisahihishe makosa
nimechofanya.
Sarah, mtu wangu-- safi kabisa. Uko mbele ya 'majaribio' ya sentensi. Unmetunga makala vizuri kabisa! Naweza kusahihisha kidogo tu, (mara nyingi napata msaada wa boss/mume/mkuu/ kifaru... wangu kwenye masahahisho...mwenyewe lazima niwe na makosa kadha pia.
ReplyDeleteNeno la mwisho "nimechofanya" na kati kati umeandika "nimechopanga" ningebadilisha kusema "niliyofanya" na " "nilivyopanga". Mara nyingi tense ya hiyo construction ni "li" au "na", sio "me".
Pia "vyo" au "yo" hutumika sana, ila inaendana na ngeli kabla ya neno lenyewe. Kwa hiyo "nisahihishe MAkosa niliYofanya. / niletee KITI uliCHOsafisha.
wako,
Anna
Asante sana, Anna! Napenda kusahihishwa na watu ambao wanajua kiswahili sanifu kwa sababu siku hizi nataka nisiwe mvivu kuongea. Vilevile ninatarajia kurudi kijijini itabidi niboreshe kiswahili changu ili niwasiliane na wenyeji. Mungu akipenda nitashinda!
Delete